NEWS ALERT; WANAFUNZI WA INFORMATICS KUTOKA UDOM WAENDELEA NA MAANDAMANO NA MGOMO WAO JIONI HII - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NEWS ALERT; WANAFUNZI WA INFORMATICS KUTOKA UDOM WAENDELEA NA MAANDAMANO NA MGOMO WAO JIONI HII

 
 Wanafunzi Wa Kitivo Cha Mawasiliano Kutoka Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakusanyika Mbele Kuongea Na Principle Wa Kitivo Chao Muda huu.Kwa Maalengo yakutaka kupewa fedha zao za Kitivo Maalumu (Special Faculty) ambapo Walikuwa wanapewa Tsh 50000 badala Ya Tsh 850000.Ambapo Jana Wanafunzi Hao Waliandamana Ili Kufika Ofisi Za Waziri Mkuu Na Hawakufanikiwa.
Baadhi Ya Wanafunzi Wa Kitivo Cha Mawasiliano (Informatics) Wakimsikiliza Principle (Wa Pili Kushoto) Wa Kitivo Chao Mara Baada Ya Kukusanyika Mbele Ya Ukumbi Chimwaga uliopo Chuoni hapo.

Wanafunzi Wa Kitivo  Cha Informatics Walipokua Wakiimba Nyimbo za Kimapinduzi Mbele Ya jengo la Chimwaga Jioni Hii Huku Wakimwaga Maji Juu.

Wanafunzi Hao wamekuwa Wakilalmika Ili Kupewa fedha zao za Kitivo bila mafanikio na Sasa Wanafunzi hao wameendelea na maandamano yao tokea jana na sasa wameamua kukusanyika mbele ya Ukumbi Wa Chimwaga Mpaka Muda huu tunaingia mitamboni wanafunzi hao Bado wapo Mbele ya Ukumbi wa Chimwaga Wakimsikiliza Principle wao japokuwa wakionyesha kutokukubaliana nae. Wakati huohuo Vijana Wa Mwema Tayari Wakiwa Tayari Kukabiliana na Hali yoyote ambayo inaweza Kuhatirisha Amani Chuo Hapa.Tuvute Subira Na Tutaendelea Kujuzana.

1 comment:

  1. Jembe5:55 PM

    Tunasikitishwa saaaaaana na SISA ya chuo hiki cha UDOM shida si wanafunzi, bali MANAGEMENT nzima ya chuo hiki. Yaaani ni SIASA na UDINI kwa kwenda mbele ndio maana maendeleo yetu hatuyaoni.
    USHAURI:
    Ikiwezekana uongozi mmbovu ndani ya chuo ubadilishwe ilikukuza taaluma ya WASOMI tuliopo chuoni hapa.
    Binafsi naumwa saaaaaaaaaaaanna na ROHO.

    EE MUNGU TUSAIDIE WANAO WA UDOM

    ReplyDelete

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages