DIRECTOR MKONGWE WA MUVI AAGWA, KUZIKWA MOROGORO LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

DIRECTOR MKONGWE WA MUVI AAGWA, KUZIKWA MOROGORO LEO

Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Tanzania (basata), Ghonje Materego (wa pili kushoto), akisikiliza maelezo mafupi kuhusu kifo cha Director Mkongwe wa muvi nchini, Hammie Rajab, aliyefariki alfajiri ya kuamkia leo katika hospitali ya Amana. Marehemu ameagwa hospitalini hapo kwenda Mororgoro ambako anatarajiwa kuzikwa jioni hii. Marehemu aliyekuwa na umri wa miaka 75, ameacha mke, watoto 14 na wajukuu 14. Mungu ailaze roho ya marehemu peponi, Amin!
Msanii wa filamu nchini maarufu kwa jina la Mzee Chilo, akisalimiana na Juma Mbizo wakati wa kumuaga marehemu katika hospitali ya Amana.
Katibu Mkuu wa basata, Bw. Materego (kati) akibadilishana mawazo na Mbizo msibani hapo, kushoto ni afisa Habari wa basata, Aristedes Kwizela
Mtangazaji wa kipindi cha EATV cha Bongo Mivies, Joyce Kiria (kulia) akiongea jambo na Mzee Chillo, mmoja wa wasanii waliocheza filamu ya mwisho kutengenezwa na marehemu, Tears On Valentine Day
Katibu Mkuu wa Basata akiongea na Star TV
Farid Hammie Rajab, mtoto wa pili wa marehemu (wa kwanza kulia), akiongea na Mkurugenzi wa kampuni ya video ya XL, BW. Ibrahim, ambaye alikuwa akifanyakazi pamoja na marehemu
...Wanahabari wa Star TV
...marehemu akibebwa kuelekea kwenye gari tayari kwa safari ya Morogoro
...ni wakati wa vilio na majonzi
...duaa kwa marehemu
Farid Hammie(kulia) akipewa pole na Musa kutoka TruVison Company ya jijini Dar
...safari ya kuelekea Morogoro ilianzia hapa.

PICHA: Haroun Sanchawa/GPL

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages