MUSWADA WA KATIBA MPYA WASOGEZWA MBELE ILI KUJADILIWA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MUSWADA WA KATIBA MPYA WASOGEZWA MBELE ILI KUJADILIWA


Spika wa Bunge Anne Makinda akizungumza Bungeni mjini Dodoma.
-
Na.Mwandishi wetu,Dodoma.
Bunge limesimamisha mjadala wa muswada wa marejeo ya mabadiliko ya Katiba mpya, na kuiagiza serikali kuandaa upya ukiwa katika lugha ya kiswahili.
Pia, limeagiza muswada huo kuchapishwa na kutangazwa katika vyombo vya habari ili kutoa fursa ya kutosha kwa wananchi kuusoma na kuuelewa kabla ya kutoa maoni yao.
Tamko hilo limetolewa bungeni leo na Spika wa Bunge Anne Makinda, baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, iliyokuwa ikisimamia kuratibu maoni ya wananchi.

Muswada huo uliwasilishwa bungeni kwa hati ya dharura, ambapo baada ya kusomwa Bunge liliandaa utaratibu wa wananchi na wadau kutoa maoni katika vituo vya Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar.

Hata hivyo, kinyume na ilivyotarajiwa kazi ya utoaji maoni ilizusha vurugu na watu kurushiana maneno huku baadhi ya wanasiasa wakidaiwa kuhusika kupotosha wananchi.
Spika Anne alisema Aprili 13, mwaka huu, Kamati hiyo ambayo iko chini ya Mwenyekiti wake Pinda Chana, iliwasilisha taarifa ya maelekezo ya awali juu ya muswada huo ulivyofanyiwa kazi na kutoa mapendekezo kadhaa.

Alisema kwa mujibu wa kanuni 2(2) ya Kanuni za Bunge Toleo la 2007, inatoa mamlaka kwa Spika kuamua utaratibu wa kufuata iwapo Kamati iliyopelekewa Muswada haitakuwa imekamilisha kazi kwa muda husika.

Spika Anne alisema kutokana na ushauri huo, iliamualiwa kuwa muda zaidi utolewe kwa Kamati na wananchi kuufikiria muswada huo.

Pia,alisema muswada huo unatakiwa kuwekwa vizuri zaidi ili wananchi waweze kuelewa madhumuni yake.

Anne alisema imeonekana wazi kuwa wananchi wengi wamedhani tayari serikali imeanza kuandika katiba, wakati kilichofanyika ni kutunga sheria ya kuunda Tume ya kukusanya maoni tu.
“Nimeridhika na mapendezo yaliyotolewa na nimeona busara kutoa muda zaidi ili kazi ya kuuchambua muswada huu iendelee. Pia,kuendelea kukusanya maoni ya wadau na kuyachambua ili kuuboresha zaidi na uwe na manufaa kwa taifa,” alisema Spika Anne na hapo ukumbi ukalipuka kwa furaha.

Hata hivyo,Spika Anne alionya kuwa muswada huo si mali ya chama chochote cha siasa na kwamba,watatumia busara ya kutoa mawazo kikamilifu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages