MREMA KUPAMBANA NA VIONGOZI WABOVU VIJIJINI, TARAFA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MREMA KUPAMBANA NA VIONGOZI WABOVU VIJIJINI, TARAFA

 
Mrema akisisitiza jambo katika mkutano huo.
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Augustino Mrema, ameshutumu utendaji mbaya wa viongozi wa serikali katika vijiji na tarafa na kuahidi ataanza kuwachukulia hatua.

Akiongea na waandishi wa habari katika Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam, Mrema ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party, alitoa mfano wa utendaji mbaya wa viongozi waliopewa majukumu ya kugawa pembejeo za kilimo na misaada mingine ya serikali.

Alisema wahusika wanafanya kinyume cha wajibu wao kwa kuwa wameweka maslahi yao mbele hivyo kuhujumu mipango hiyo.

PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages