Ukumbi Wa Chimwaga Uliopo UDOM
Chuo Kikuu Cha Dodoma Kina Takribani Vitivo Vinne sasa vinavyofanya Kazi Vikiwemo Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii , Sanaa na Lugha, Kitivo Cha Elimu, Kitivo Cha Udaktari na Kitivo Cha Teknolojia Ya Habari Na Katika Vitivo hivi kila Kitivo Kina Uongozi Wake Wa Wanafunzi Ambapo Kunakua na Raisi Au Mwenyekiti Wa Kitivo Na Makamu wake Lakini Vilevile Kuna Nafasi Ya Raisi Wa Chuo Kizima Cha Dodoma Ambapo Kila Mwaka Wa UChaguzi Huwa Anatoka Katika Kitivo Tofauti Tofauti, Zamu Hii Ya Uchaguzi Mwaka Huu Anayewania Nafasi Ya Uraisi Wa Chuo Kizima Anatoka Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii Sanaa Na Lugha Ambapo Sasa Baadhi Ya Wanaowania Nafasi hizo za Uraisi na Makamu Wa Raisi Tayari Wameshaanza Kufanyiwa Interview Na Tume ya Uchaguzi Ya Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii, Sanaa na Lugha Kwa ajili ya kupata Majina mawili ambayo yatapigiwa Kura na Wanafunzi. Mpaka Sasa Waliojitokeza Kuwania Nafasi Ya Uraisi Wa Chuo Kizima Yaani UDOSO FEDERATION ni Watahiniwa 10 Ambapo Wawili tu Ndo wanahitajika Ili Waweze kupigiwa Kura na Waliojitokeza Kuwania Makamu Wa raisi wa UDOSO FEDERATION ni Wawili
Ndani Ya Ukumbi Wa Chimwaga Uliopo Chuo Kikuu Cha Dodoma(Picha Kutoka Maktaba)
Vile Vile Waliojitokeza Kuwania Nafasi ya Uraisi Wa Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii Sanaa Na Lugha Ni Zaid Ya 15 ambao wamefanyiwa Interview majira ya asubuhi ambapo na katika nafasi hiyo pia ni wawili tu ndio wanaohitajika ili waweze kupigiwa kura Na Wanafunzi. Interview Hiyo Inafanyika Hivi Sasa Katika Chumba Kimoja Kilichopo Katika Ukumbi Wa Chimwaga
Zahanati Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma.
Hali Kwa Sasa Ni Shwari Ambapo inatarajiwa kuwa baada ya Majina kupitishwa Na Wagombea wa nafasi mbalimbali kujulikana basi kampeni zitaanza mara moja.Tayari Kama Unavyoelewa Kuna Mambo ya hapa na pale katika kampeni Ambayo huwa hayakosi kutokea Kama Kuanza Kashfa na Fitina ili kusudi mmoja aonekane mbaya na mwingine mzuri.Picha Zote Kutoka Maktaba
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)