MAREHEMU FIVE STAR WAFANYIWA KISOMO CHA AROBAINI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAREHEMU FIVE STAR WAFANYIWA KISOMO CHA AROBAINI

 
Mbunge wa  Temeke, Zuberi Mtemvu, ( kushoto) na  Mbunge wa Ilala, Iddi  Hassani Zungu wakisoma dua.
WANAMUZIKI 13 wa kundi la muziki wa taarabu la Five Star waliofariki katika ajali ya gari katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Morogoro,  mwezi  Machi mwaka huu, jana walifanyiwa hitma katika  ukumbi wa PTA uliopo katika Viwanja vya Maonyesho ya Biashara vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.  Miongoni mwa mamia ya watu waliohudhuria ni pamoja na Mbunge wa  Temeke, Zuberi Mtemvu,  na Mbunge wa Ilala Hassani Zungu.

 
Baadhi ya watu wakiwasili  katika hitma hiyo.
 
Mbunge wa Temeke, Zuberi Mtemvu (katikati) akiongea jambo na mwanamuziki  Matei Joseph (kushoto) na Saidi Fela mara baada ya kuwasili.
 
Miongoni mwa mamia waliojitokeza katika kisomo hicho.
 
Mwanamuziki wa bendi ya TOT Taarab, Khadija Omar Kopa (kushoto) akiongea na meneja wa TMK Wanaume Family, Saidi Fela.
 
Khadija kopa (kushoto) akiwa na Mwanahawa Ally mwanamuziki aliyenusirika katika ajali hiyo.
 
Zuberi Mtemvu ( kushoto) na Iddi Hassani Zungu wakifuatilia kisomo hicho.
 
...Wakipata  msosi.
 
Baadhi ya waalikwa wakitoka nje baada ya kisomo hicho.


PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY / GPL

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages