Mke wa Rais mama Salma Kikwete akiongea na wakazi wa wilaya ya Nanyumbu (hawapo pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi wa jengo la wodi ya wazazi katika kituo cha Afya Mangaka ambapo pamoja na mambo mengine ametoa wito kwa akina mama wajawazito nchini kujitokeza kupata huduma za afya ya uzazi katika vituo vya afya vilivyopo ili kuepuka matatizo ya uzazi yakiwemo vifo vya mama wajazito.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) mama Salma Kikwete akiwa amembeba mtoto mchanga aliyezaliwa akizungumza na Bi.Rehema Twaribu (kushoto) mmoja wa wanawake waliopata huduma ya Afya ya Uzazi katika kituo cha Afya Mangaka.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) katikati akikata utepe akiwa na watendaji wa shirika la EGPAF la Marekani lililowezesha upatikanaji wa jengo hilo kwa kushirikiana na wizara ya afya nchini kuashiria uzinduzi wa jengo la wodi ya wazazi la kituo cha Afya Mangaka wilayani Nanyumbu, Wa pili kutoka kulia ni mkurugenzi mkazi wa shirika la EGPAF nchini Bw. Jeroen Van’t Bosch.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo –WAMA (kushoto) akizungumza jambo na watoto waliofika kushuhudia uzinduzi wa jengo la wodi ya wazazi katika kituo cha Afya Mangaka wilayani Nanyumbu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)