MADEREVA WA MALORI WAZIBA NJIANI KUPINGA USHURU WA 15,000 KWA AJILI YA MAEGESHO YA MILLENIUM BUSINESS PARK - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MADEREVA WA MALORI WAZIBA NJIANI KUPINGA USHURU WA 15,000 KWA AJILI YA MAEGESHO YA MILLENIUM BUSINESS PARK


Baadhi ya wafanyabiashara walio na ofisi ndani ya majengo hayo wakiwa nje, baada ya kushindwa kupitisha magari yao kuingia ndani. Wahindi wanaodaiwa kuanzisha utaratibu huo wakisimamia magari katika geti la pili baada ya kufunguliwa huku wakiwakomand walinzi kuruhusu magari bila kuandikishwa getini hapo kinyume cha utaratibu.
Wahindi hao wakilinda mlango wa Meneja aliyekuwa amejifungia ndani ambapo hatutaka kuonana na mtu.
Baadhi ya wafanyabiashara hao wakijadiliana nje ya ofisi hizo kutafuta ufumbuzi wa kupitisha magari yao.
Baadhi yao walianza kuhamisha vitendea kazi vyao katika ofisi hizo ili kuendelea na kazi zao katika mahala pengine walikotafuta kwa muda.
Hili ndilo geti la pili la kutokea ambalo pia lilikuwa limefungwa na malori hayo, kama unavyoona gari hilo lilivyokaa getini hapo kwa kukatiza njia ili gari jingine lisiweze kupita.
Wapakuaji mizigo wakiwa nje ya magodauni hayo wakisubiri kukamilika kwa utaratibu ili magari yaingie waanze kazi ya kushusha mizigo.
Huku ni uapnde wa pili wa geti la kutokea pia kukiwa na foleni kutokana na Lori hilo kuziba njia. Madereva wa malori hayo waliegesha magari hayo toka juzi jioni walipofika kwa ajili ya kupakua mizigo na kukuta utaratibu huo uliowekwa na wamiliki kinyume na mkataba wa wapangaji.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages