CHADEMA YAMNADI MGOMBEA UDIWANI WADI YA MWANYANYA JI MBO LA BUBUBU ZANZIBAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

CHADEMA YAMNADI MGOMBEA UDIWANI WADI YA MWANYANYA JI MBO LA BUBUBU ZANZIBAR


Katibu wa Chademba jimbo la Bububu Zanzibar, Yusuf Khatibu Miraji (pichani) ametoa malalamiko kwa uongozi wa juu wa chama hicho kutokana na kuwapa fedha kidogo, sh.500,000/- kufanyia kampeni za uchaguzi wa diwani wadi ya Mwanyanya ambapo uchaguzi ulifanyika Jumapili.

"Tuliomba sh.8,000,000/- kwa kampeni pamoja na kuwalipa mawakala wetu, sasa bwana mwandishi kiasi hicho kidogo kitafaa nini katika hali hii ya ushindani? Angalau wangetupatia nusu ya fedha tulizoomba." Alisema Katibu huyo kwa masikitiko makubwa na kukata tamaa ya ushindi kwa mgombea wao wa udiwani Salum Omar Abeid.
Mjumbe wa Kamati Kuu na aliyekuwa mgombea mwenza wa Chadema, Said Mzee Said (kulia) akimtambulisha kwa wananchi, mgombea udiwani kupitia chama hicho, wadi ya Mwanyanya jimbo la Bububu Zanzibar, Salumu Omar Abeid kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Jazira juzi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages