WAZIRI MKUU ATEMBELEA WAATHIRIKA WA MABOMU JANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAZIRI MKUU ATEMBELEA WAATHIRIKA WA MABOMU JANA

Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) akizungumza na baadhi ya familia za waathirika wa milipuko ya mabomu eneo la Majoe jana jijini Dar es salaam na kuwahakikishia kuwa serikali itafanya kila linalowezekana kuwasaidia.Picha zote na Aron Msigwa-MAELEZO Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akizungumza na wakazi wa Gongolamboto (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kuwaona waathirika wa milipuko ya mabomu iliyotokea katika kambi ya JWTZ Gongolamboto jana jijini Dar es salaam ambapo ametoa wito kwa mamlaka zinazohusika na ugawaji wa misaada kuhakikisha kuwa misaada hiyo inawafikia walengwa.
Wajasilia mali wa kikundi cha SEUMA kutoka Segerea jijini Dar es salaam wakimkabidhi Waziri mkuu Mizengo Pinda msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa milipuko ya mabomu ya Gongolamboto jana jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages