WANA WA AFRIKA MASHARIKI WAREJEA KUTOKA LIBYA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WANA WA AFRIKA MASHARIKI WAREJEA KUTOKA LIBYA


Kenya
Watu 151 raia kutoka Kenya, Tanzania , Uganda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Lesotho wamewasili nchini Kenya wakitokea Libya, kukimbia machafuko.
Raia wa Afrika Mashariki wakiwasili Nairobi
Watu hao wamewasili kwa shirika la ndege la Kenya, baada ya safari yao kucheleweshwa kwa muda wa saa 24 kutokana na kukosa kibali cha kutua kwenye uwanja wa ndege wa Tripoli.
Wengi wa watu hao walikuwa wanahofia maisha yao kufuatia mashambulizi dhidi ya raia wakigeni nchini humo.
Mwandishi wetu Anne Waithera alikuwepo kwenye uwanja wa ndege wa Jomo kenyatta amesema walionekana wachovu, huku wengine wakikataa kuzungumza na waandishi wa habari, wakitaka kwenda majumbani mwao tu.
Tanzania
Mmoja wa watanzania aliyerejea kutoka Libya
Mwandishi wetu anasema si wengi walikuwa na jamaa zao wakiwasubiri uwanjani hapo.
Balozi wa Libya nchini Kenya aliyekuwepo uwanjani hapo amesema barabara za kwenda na kutoka kusini mwa nchi na hata kuelekea Benghazi zimefungwa.
"Tunawasiliana na serikali za Marekani na Uingereza kutazama hali ilivyo. Lakini Wakenya wote waliobaki huko wako salama". amesema.
Tanzania
Mtanzania aliyerejea kutoka Libya
Aggrey Simiyu, raia wa Kenya alisema anafurahi kurejea nyumbani. "Tulivamiwa na watu, na salama yetu ilikuwa baada ya kuwakabidhi funguo za gari" amesema.
Bw Simiyu amesema walikuta vizuizi vingi barabarani, na kila mara walikuwa wakikaguliwa. "Tulinyanganywa simu zetu pia." amesema.
Balozi za nchi zingine zilizoko nchini Kenya sasa zinapanga jinsi raia wao waliowasili Nairobi leo watasafirishwa hadi nyumbani kujumuika na jamii zao baada ya matatizo yaliowakabili.
Chanzo BBC SWAHILI.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages