WATU 3000 WAKADIRIWA KUNYWA DAWA YA BABU WA LOLIONDO KWA SIKU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WATU 3000 WAKADIRIWA KUNYWA DAWA YA BABU WA LOLIONDO KWA SIKU


Dawa Ikiwa Kwenye Sufuria ikichamshwa kwaajili ya Kutibu watu
Baadhi ya watu waliokunywa dawa hizo wakiwa wamelala kupumzika nyumbani kwa Babu huyo.
Hii ndiyo dawa yenyewe ikiwa tayari kwa kuywewa baada ya kucheshwa
Na Mwandishi Wetu, Loliondo
WAKATI watu zaidi ya 3,000 wakiendelea kufurika kila siku kunywa dawa Mchungaji Ambilike Mwasapile amesema bado ataendelea kuwa fiti kuhudumia watu watakaofika nyumbani kwake.

Mbali na kueleza kwamba bado yupo ‘gado’ Mchungaji huyo ametoa onyo kali kwa wajasiriamali na watu wenye magari ya kubeba abiria kwa vitendo vya kupandisha huduma hadi kiwango cha kutisha.


Akizungumza nyumbani kwake na vyombo vya habari juzi Mchungaji Mwasapile, alisema, hivi sasa zaidi ya watu 3,000 wanakwenda nyumbani kwake katika Kijiji cha Samunge wilayani Ngorongoro kwa ajili ya kunywa dawa kwa gharama ya Sh 500 kama alivyoagizwa na Mungu katika ndoto.
“Watu ni wengi wanakimbilia uponyaji na hawa bado ni tone katika wale wanaondelea kuja hapa, nisingependa kuona wafanyabiashara wakianza kuwamiza watu wanaokuja kunywa dawa.


“Hii ni agizo kutoka kwa Mungu kwamba dawa hii itolewe kwa kiwango cha Sh 500 kwa hiyo hata wao wanapaswa kuwatoza gharama za kawaida kabisa watu wanaokuja huku,” alisema Mchungaji Mwasapila ambaye hivi sasa amejizoelea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi.


Onyo la Mchungaji Mwasapile limekuja muda mfupi baada ya umati wa watu kukimbilia katika Kijiji cha Samunge ambacho kipo umbali wa takribani kilomita 400 kutoka Arusha mjini, ambapo ili kufika huko ni lazima abiria watumie usafiri wa magari aina ya Toyota Landcruiser na mabasi.
Nauli za magari kuelekea kijijini Samunge zimefika kiasi cha Sh.100,000 hadi 130,000 kwa mtu mmoja kwa safari ya kwenda na kurudi wakati nauli ya zamani ilikuwa ni Sh. 37,500. Na kwa upande wa magari aina ya Landcruiser imepaa hadi kufikia Sh. 150,000 na 200,000 kwa mtu mmoja kutoka Sh. 35,000.
Kwa upande wa bei ya vyakula kijijini hapo imezidi kupaa na kufikia Sh.1000 kwa sahani hadi Sh. 3000 kwa sahani ya chakula, wakati nyama ya mbuzi ya kuchoma ikipanda kutoka Sh.4000 kwa mguu hadi Sh. 20,000.Wakati maji ya kunywa yakiuzwa kwa Sh. 1,000 hadi Sh. 1,500 kutoka Sh. 500 sanjari na soda.
Wakizungumzia ongezeko hilo pamoja na Mchungaji Mwasapile akitoa onyo kali kwa watoa huduma hiyo kushusha bei haraka, baadhi ya watu waliokwenda kunywa dawa walisema kwamba kwa sasa wafanyabiashara wamegeuzia gharama za dawa hiyo kwenye mahitaji ya kibinadamu.


“Unajua binadamu tuna matatizo sana Mchungaji amepewa huduma hii na Mungu bure nay eye ameamua kutoa bure, lakini imefika kwetu waananchi wanaona hapa ndoiuo mahali poa kutajirikia jambo hili si sahihi kabisa.
“Sasa hii yote inatoa taswira kwamba kama ingekuwa si Mungu ndani ya Mchungaji na zawadi hii akapewa mtu mwingine au ikawa ni geresha kwa watu hakika wangekuwa wanaitoa dawa hii kwa gharama kubwa haijawahi kuonekana,”alisema Joseph Mwangosi.


Hata hivyo baadhi ya watu wengine waliomba serikali kuingilia kati kwa kusimamia bei za bidhaa katika eneo hilo kwani zitazidi kuwaumiza zaidi ilhali wao wamekwenda kwa ajili ya kupata huduma ya dawa..

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages