DEREVA SHALOBALO ATUNISHA MISULI BAADA YA KUSABABISHA AJALI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

DEREVA SHALOBALO ATUNISHA MISULI BAADA YA KUSABABISHA AJALI

Dereva wa gari ndogo yenye namba za usajiri T 180 BHX, anayeonekana pichani (kulia) akiwa nyuma ya gari lake baada ya kumchomekea dereva wa Daladala linalofanya safari zake Mwenge Kariakoo, lenye namba za usajiri T534 AEA, maeneo ya Mwanamboka jana usiku
Askari wa usalama Barabarani, akipima ajali hiyo upande wa Daladala.
Daladala hilo likiwa limeingia mtaroni maeneo hayo kutokana na ajali hiyo.
 
 Ajali iliyopelekea daladala hiyo kupanda ukuta na kuingia mtaroni hadi kutokea upande wa pili wa Barabara hiyo. Dereva huyo imeelezwa kuwa baada ya ajali hiyo alitelemka ndani ya gari lake na kuanza kumkoromea dereva wa daladala huku akijitamba kuwa yeye ni mkubwa Serikalini. Dereva huyo bila kujua anazungumza na Sufianimafoto alimfuata Sufianimafoto na kuanza kumkolomea "kwanini unapiga picha gari yangu bila ruksa yangu Meen" Sufianimafoto hukua kiendelea na kunasa matukio alijaribu kumuelewesha taratibu za kazi yake na kumwambia mbona huyu askari wa usalama Barabarani hawaki kupigwa picha wakati akifanya kazi ya kupima ajali iweje wewe?" lakini bado jamaa huyo alizidi kujigamba. "Unajua mimi ni nani huyo askari ni mtu mdogo saana kwangu mie, acha kupiga picha husikii?" aliwaka na kuanza kutukana matusi ya nguoni huku akishika suluali yake ya jinzi chini ya naniliu kama wafanyavyo watu wa kufoka foka wawapo jukwaani, lakini hiyo haikumtishia nyau Sufianimafoto kwani aliendelea na kazi yake hadi aliporidhika na kuondoka zake na kumuacha Shalobalo huyo akimtolea mimacho tu asijue cha kumfanya. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages