VIINGILIO MECHI YA YANGA NA SIMBA VYATANGAZWA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

VIINGILIO MECHI YA YANGA NA SIMBA VYATANGAZWA LEO

 
Mechi namba 108 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya wenyeji Yanga na Simba itachezwa Jumamosi (Machi 5 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni kama ifuatavyo;

Viti vya kijani mzunguko ambavyo viko 19,648 ni sh. 3,000

Viti vya bluu mzunguko (17,045) ni sh. 5,000

Viti vya rangi ya chungwa (11,897) ni sh. 7,000

VIP C yenye viti 4,060 ni sh. 10,000

VIP B yenye viti 4,160 ni sh. 20,000

VIP A yenye viti 748 ni sh. 30,000

Tiketi zitaanza kuuzwa Ijumaa saa 2 asubuhi katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Big Bon Msimbazi (Kariakoo), Mgahawa wa Steers uliko Mtaa wa Samora/Ohio na Uwanja wa Uhuru.

Pia siku ya mchezo tiketi zitaendelea kuuzwa katika maeneo hayo kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 6 mchana. Baada ya muda huo zitaendelea kuuzwa Uwanja wa Uhuru pekee.

Mwamuzi atakuwa Oden Mbaga wa Dar es Salaam akisaidiwa na Mohamed Mkono (Tanga) na Maxmillian Nkongolo wa Rukwa. Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Mchungaji Army Sentimea wa Dar es Salaam.

Boniface Wambura
Ofisa Habari

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages