MGAMBO ALIPOGEUKA KUWA ASKARI WA USALAMA BARABARANI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MGAMBO ALIPOGEUKA KUWA ASKARI WA USALAMA BARABARANI

Askari wa Jiji wa Manispaa ya Ilala, wakimdhibiti kijana dereva wa Pikipiki, aliyekuwa akijaribu kubishana na kumkoromea mgambo wa kushoto, asiondoke na pikipiki yake baada ya kuanza kuikokota na kutaka kuondoka nayo kutoka eneo la Shule ya Uhuru kwa kile walichodai pikipiki hiyo iliegeshwa katika eneo lisiloruhusiwa.
Kijana huyo alisikika akijitetea kuwa yeye si dereva wa Bodaboda bali ni mpita njia aliyekuwa amesimama eneo hilo kwa lengo la kuzungumza jambo na mwenzake aliyekutana naye kwa ghafla eneo hilo na kuamua kuzima pikipiki huku wakiendelea kupiga stori wakiwa pembeni mwa pikipiki hiyo.
 
Hali hiyo ilimstua kijana huyo baada ya kustukia tu mgambo huyo akitokea nyuma yao na kuanza kulazimisha kuikokota wakati ikiwa kwenye gia na kumshinda.
Baada ya vurugu la dakika kadhaa pikipiki hiyo ilianguka na kuanza kuvuja mafuta huku raia waliojazana mahala hapo wakimzomea mgambo huyo kwa kushindwa hata kuikokota pikipiki hiyo, huku wengine wakisema "kwani we ni Trafic hiyo ni kazi ya Trafic" walisema wapitanjia. Hapa wakijaribu kunyang'anyana pikipiki hiyo hali iliyoifanya pikipiki hiyo kuanguka kwa kishindi na kuanza kuvuja mafuta.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages