Spika Makinda akitioa mada kuhusu Ushirikishwaji wa Jinsia katika Vyama vya Siasa katika mkutano huo nchini Liberia.
Mwenyekiti wa Taifa wa tume ya Uchaguzi Mh. James Fromoyan, Spika Makinda na Seneta Clarice Jah wakifuatilia kwa makini mada ya Waziri wa Jinsia na Maendeleo wa Liberia Mh. Varbah Gayflor (hayupo kwenye picha)
Spika Makinda akitambulishwa kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Liberia, Mhe. James Fromoyan (kulia)na hatimaye kufanya mazungumzo ya pamoja.
Spika wa Bunge la Tanzania Mh. Anne Makinda (wa pili kutoka kulia) akiwasili katika ukumbi wa Mkutano wa kuhamasisha ushirikishwaji wa wanawake katika vyombo wa kutoa maamuzi unaoendelea mjini Gbarnga, Liberia kwa mwaliko wa Taasisi ya Kimataifa inayosaidia uimarishaji wa Demokrasia na Chaguzi huru(International Institute for Democracy and Electoral Assistance-IDEA). Kulia kwake ni mwenyeji wake na ni Mwenyekiti wa Taifa wa Wabunge Wanawake nchini Liberia Seneta Carice A. Jah akimtambulisha Spika kwa viongozi wa wa chama cha wanawake wabunge wa Liberia
Spika Makinda akiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake wa Liberia.Habari na Picha na Prosper Minja – Bunge
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)