Mkuu wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Morogoro (RTO) Ibrahim Mwamakula akitazama Gari la mkuu wa mkoa wa Morogoro. |
Mti uliogongwa na gari ya mkuu wa mkoa |
Maafisa wa polisi wakiangalia pikipiki iliyosababisha ajali |
MKUU wa mkoa wa Morogoro Issa Machibya amenusuriki kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali katika eneo la kwa Mnyonge barabara ya zamani ya Old Dar es Salaama baada ya kugonga mti wakati dereva wa gari hiyo akimkwepa mwendesha pikipiki kabla ya kuachia njia na kuingia katika mashamba ya mpunga.
Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 11 alasiri machi 15 ilihusisha pikipiki yenye namba za usajili T734 BMK Sunlg na gari la mkuu huo wa mkoa ambalo lilikuwa likiendesha na dereva Abeid Namangasa (43) ikitokea Bigwa kuelekea mjini ambapo mwendesha pikipiki aliyetambuliwa kwa jina la Edwin Rugambwa (33) mkazzi wa Kichangani mkoani hapa kudaiwa kubadilisha mwelekeo ghafla hali iliyomchnganya dereva wa gari la mkuu wa mkuu wa mkoa
Akizungumza eneo la ajali dereva wa mkuu wa mkoa Abeid Namangasa (43) alisema kuwa ajali hiyo ilisbabishwa na dereva wa pikipiki kwa kukata kona na kurudi alikotoka wakati huo gari yake tayari ilikuwa ipo jirani naye na kulazimika kumkwepa ili nisimgonge. (Picha:Juma Mtanda wa Morogoro)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)