MIRIAMU LUKINDO AFANYA MKUTANO NA WANAHABARI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MIRIAMU LUKINDO AFANYA MKUTANO NA WANAHABARI

 
Miriamu akiwaelezea waandishi wa habari jinsi uzinduzi wake utakavyokuwa.
MUIMBAJI wa nyimbo za injili nchini, Miriamu Lukindo leo amefanya mkutano na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari katika Mgahawa wa Hadees uliopo Posta jijini Dar es Salaam, akiwaeleza maandalizi ya uzinduzi wa  albamu yake  aliyoipa jina la Ni Asubuhi.

Miriamu amesema uzinduzi huo utakafanyika Aprili 10, 2011 ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. 

 
Miriamu akiwa pamoja na Mratibu wa tamasha lake, John Momadi ( wa kwanza kulia) pamoja na Meneja wake, Humphery Maziba wakiwa tayari kwa ajili ya kuongea na waandishi  wa habari kuhusu uzinduzi huo.
 
Mratibu wa uzinduzi huo, John Momadi akizungumza jambo.
 
Miriamu akiwa na kamati ya maandalizi ya uzinduzi huo.

Stori/Picha: Imelda Mtema / GPL

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages