MAN U YAFIA DARAJANI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAN U YAFIA DARAJANI

LONDON, England
BAO la mkwaju wa penalti lililofungwa na Frank Lampard limeiwezesha Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester United.

Mabingwa hao wa England waliibuka na ushindi katika mechi hiyo ya kiporo iliyochezwa usiku wa kuamkia leo kwenye Uwanja Stamford Bridge jijini London.

Matokeo hayo yameiweka Chelsea katika nafasi ya nne kwa kuwa na pointi 48 huku Man United ikiendelea kujikita kileleni kwa kuwa na pointi 60. Chelsea ina mchezo mmoja mkononi.
 
Man United ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 29 lililofungwa kwa shuti kali na Wayne Rooney aliyepokea pasi ya Luis Nani na kuwahadaa mabeki wa Chelsea kabla ya kuachia ‘bunduki’.

Kipindi cha pili Chelsea ilibadilika na kuonyesha uhai hasa katika sehemu ya kiungo na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 54 mfungaji akiwa David Luiz raia wa Brazil. Luiz alifunag bao hilo kwa shuti kali baada ya kudondoshewa mpira wa kichwa na Branislav Ivanovic.

Kosa lililofanywa na beki Chris Smalling wa Man United katika dakika ya 78 la kumzuia ‘njiani’ Yuri Zhirkov ndani ya eneo la hatari lilisababisha penalti iliyopigwa na Lampard dakika ya 79 na kuzaa bao la pili na la ushindi kwa Chelsea.

Katika mchezo huo uliotawaliwa na ushindani pamoja na jazba kwa wachezaji wa pande zote mbili, beki wa Man United Nemanja Vidic alionyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi Martin Atkinson baada ya kumvuta jezi Ramires.

Chelsea ilifanya mabadiliko ikiwa ni pamoja na kumuingiza Didier Drogba badala ya Nicholas Anelka, Man United wakawaingiza wakongwe Ryan Giggs na Paul Scholes. mwisho wa mchezo ngoma ikabaki 2-1.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages