MABOHORA WAMFANYIA SHEREHE YA KUZALIWA SHEIKH WAO KWA MAANDAMANO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MABOHORA WAMFANYIA SHEREHE YA KUZALIWA SHEIKH WAO KWA MAANDAMANO

 
NA DUNSTAN SHEKIDELE,GPL/ MOROGORO
WATANZANIA wenye asili ya Kiasia maarufu kama Mabohora, leo asubuhi wamefanya maandamano  ya amani mitaa kadhaa ya mji wa Morogoro wakisherehekea siku ya kuzaliwa Sheikh wao mkuu, Dk. Syedna Mohamed Burhanuddin Saheb aliyetimiza miaka 100 ya kuzaliwa leo.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wa mji wa Morogorowalishangazwa na maandamano hayo huku wakihoji kwanini wanawake hawakushirikishwa katika maandamano hayo.

Kufuatia hali hiyo, mtandao huu ulifanikiwa kuzungumza na mmoja wa Mabohora hao aliyejitambulisha kwa jina la Dk. Taibal seifudin ambapo alidai kuwa kwa mila za dini yao wanawake hawaruhusiwi kuandamana na wanaume.

"Wanawake tumewaacha msikitini nao wanaprogramu zao wanaendelea nazo pale msikitini" alisema Taibal.
Alipoulizwa mbona kuna watoto wadogo wa kike wameshiriki maandamano hayo wakiwa juu wa roli alisita kujibu na kumtaka mwandishi wetu akazungumze na Sheikh wao wa Mkoa.Lakini jitihada za kumpata Sheikh huyo mara moja ziligonga ukuta.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages