MAPATO MECHI YA SIMBA NA YANGA NI SHILINGI MILIONI 243, 017,000 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAPATO MECHI YA SIMBA NA YANGA NI SHILINGI MILIONI 243, 017,000

Kikosi cha Yanga
KIKOSI CHA SIMBA
Tanzania Football Federation
Affiliated to FIFA, CAF and CECAFA


Karume Memorial Stadium, Uhuru/Shaurimoyo Road
P.O. Box 1574, Dar es Salaam, Tanzania . Telefax: + 255-22-2861815
E-mail:
tfftz@yahoo.com . Website: www.tff.or.tz

MAPATO MECHI YA YANGA v SIMBA
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom namba 108 kati ya Yanga na Simba lililochezwa jana (Machi 5) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 243,017,000 kutokana na watazamaji 46,539 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.
Maeneo ambayo tiketi ziliuzwa zote ni viti vya kijani 19,648 na viti vya bluu 17,045. Maeneo ambayo tiketi hazikuuzwa zote ni viti vya rangi ya chungwa (orange straight and curve), VIP C, VIP B na VIP A ambayo tiketi zilizouzwa ni 309 kati ya viti 748 vilivyopo.
Viingilio katika mechi hiyo iliyooneshwa moja kwa moja (live) na Star TV na Super Sport 9 vilipangwa kama ifuatavyo; sh. 3,000 (viti vya kijani), sh. 5,000 (viti vya bluu), sh. 7,000 (orange straight and curve), sh. 10,000 (VIP C), sh. 20,000 (VIP B) na sh. 30,000 kwa VIP A.
Baada ya kuondoa gharama za mchezo na mgao kwa uwanja, Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kila timu ilipata mgao wa sh. 51,194,793.

Boniface Wambura
Ofisa Habari

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages