Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wananchi wa CCM wa mikoa miwili ya Pemba, na kuwashukuru kwa kumchagua katika uchaguzi mkuu uliopita mwaka jana na kuwa Rais wa zanzibar katika uwanja wa Bandataka jana.
MAMA Mwanamwema Shein (Kushoto) pamoja na Dk. Maua Daftari pia walikuwepo katika mkutano uliofanyika Bandataka.
Katibu Msaidizi Wilaya ya Wete Pemba Zulfa Abdallah, akisoma risala kwa niaba ya mikoa miwili ya Pemba, wakati wa Mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi wa mikoa hiyo kwa kufanikisha uchaguzi wa huru na salama kwa kuchagua Chama Cha Mapinduzi na kuongoza katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu liopita hatimae Dk. Ali Mohamed Shein kuwa rais wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Dk. Maua Daftari mara alipowasili viwanja vya Bandataka, Chakechake kwa ajili ya kuwashukuru wanaCCM wa visiwa vya Pemba.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wakimsikiliza rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akihutubia.
Picha na Ramadhani Othman
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)