KUUAWA KWA SIMBA KIBANGULILE - MBAGALA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KUUAWA KWA SIMBA KIBANGULILE - MBAGALA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
1. Mnamo tarehe 6/03/2011 Simba mmoja aliuawa na askari Polisi Maeneo ya Kibangulile, Mbagala, jijini Dar es Salaam.

2. Baada ya kuuawa kwa simba huyo, baadhi ya vyombo habari vilitangaza kuwa wananchi wa Mbagala wanahofu kuwa bado kuna simba mwingine hajauawa.

3. Tangu tarehe 6/03/2011 Askari Wanyamapori wanaendelea kufanya msako wa simba anayehofiwa kuwepo jijini lakini bado hawajamuona na juhudi za kumtafuta simba huyo zinaendelea.

4. Wizara inatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa katika vituo vya Maliasili au Polisi mara tu watakapomwona mnyamapori yeyote akizagaa ovyo mitaani.

5. Mwisho, imethibitika kuwa kuna watu ambao waling’oa kucha 10 na kukata mkia wa simba aliyeuawa tarehe 6/3/2011 na kuondoka navyo. Wizara inamtaka yeyote aliyehusika arudishe nyara hizo katika kituo chochote cha Maliasili au Polisi, kukaa na nyara za serikali ni kinyume cha sheria.


Imetolewa na:
Felician B. Kilahama 
KAIMU KATIBU MKUU
11/3/2011

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages