DSTV NA STAR TV KATIKA MAANDALIZI YA KURUSHA LIVE MCHEZO WA YANGA NA SIMBA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

DSTV NA STAR TV KATIKA MAANDALIZI YA KURUSHA LIVE MCHEZO WA YANGA NA SIMBA LEO

Fundi mitambo wa Gari la kurushia matangazo la DSTv Zambia (kulia) akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa gari la kurushia matangazo la Televisheni ya Star Tv, wakati walipokuwa wakifunga mitambo yao katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo kwa ajili ya maandalizi ya pambano la Ligi Kuu ya Tanzania Bara la watani wa jadi kati ya Yanga na Simba litakalochezwa leo jioni kwenye Uwanja huo. Mchezo huo utakuwa ukionyeshwa live kupitia Star Tv kwa ushirikiano na DSTv.
Gari la Star Tv litakalokuwa kazini hiyo leo likisaidiana na la DSTV, likiwa nje ya uwanja wa Taifa wakati wafanyakazi wa gari hilo walipokuwa wakifunga na kuandaa mitambo yao pamoja na gari la DSTV kwa ajili ya kurusha mchezo huo wa leo.
Mafundi mitambo wa Star Tv, wakiwa bize katika gari la DSTV, wakifunga na kutandaza nyaya kuingia uwanjani.
Wakichora michoro ya jinsi wapigapicha wanavyotakiwa kukaa ndani ya uwanja huo hiyo leo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages