Golikipa wa timu wa Majimaji ya Songea, Said Mohamed, akijaribu kuokoa mpira uliokuwa ukielekea langoni kwake mbele ya kiungo mshambuliaji wa Azam Fc, Ramadhan Chombo, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa jioni hii kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Muvu hii ndiyo iliyozaa penati baada ya golikipa huyu kuonekana akimdaka miguu Chombo na kuzawadiwa kadi ya njano na kupigwa penati langoni kwake, iliyopigwa na Mrisho Ngasa kipindi cha kwanza, hadi mwisho wa mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1, kwa matokeo hayo sasa Azam itaendelea kubaki katika nafasi ya tatu huku ikiwa na jumla ya pointi 36 na Wekundu wa Msimbazi wakiendelea kubaki nafasi ya pili wakiwa na jumla ya Pointi 37 na Yanga wakiendelea kubaki kileleni, wakiwa na jumla ya Pointi 38. Golikipa wa Majimaji, Said Mohamed, akiruka kujaribu kukoa mpira wa penati uliopigwa na Mrisho Ngasa na kuandika bao la kwanza la Azam, ambalo baadaye liliweza kusawazishwa na kufanya timu hizo kutoka sare.
Mpiga picha wa Star Tv, Sarungi akiwa kazini katika uwanja huo, ambapo Televisheni hiyo ilikuwa ikirusha live bila chenga mchezo huo wa Azam na Majimaji na pia ikiwa ni sehemu ya mazoezi na uzoefu wa kujiandaa kurusha live mchezo wa jumamosi wa Watani wa Jadi Yanga na Simba, ambapo Star Tv kwa kushirikiana na Dstv, watarusha mchezo huo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)