BONANZA LA TASWA LAPAGAWISHA WAANDISHI CINE CLUB - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BONANZA LA TASWA LAPAGAWISHA WAANDISHI CINE CLUB

Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, wakichuana katika kukimbia mbio za mita 100, ambapo mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absolomon Kibanda, aliibuka kidedea baada ya kuwamwaga wahariri wenzake. 

Kila mtu alikuwa na staili yake ya kucheza masebene katika Bonanza hilo kama unavyowacheki jamaa hawa akiserebuka kana kwamba wanacheza ngoma ya Kizaramo ama Mdumange. Wengine, walikuwa ufukweni wakipata upepo wa Bahari tu kutokana na kutokuwa na mazoea ya kushiriki katika michezo yeyote.
Baadaye ilikuwa ni mbio za waandishi wa kike na katika mbio hizo, Samirah Kiango wa Uhuru Redio aliibuka kidedea.
Hata Mashalobalo pia walikuwepo si unamcheki jamaa huyu alivyotinga Jinzi lake huku akipata Biere kimtindo kwa staili yake na mkononi akiwa na akiba ya chupa mbili za Ndovu wakati anayokunywa ni Tusker, sasa sijui mchanganyiko huu ni kwa sababu ni bia za bure ama vipi, Mashalobalo wanamambo!

Na baadaye ilikuwa ni burudani ya Misebene kwa kwenda mbele, hapa wakiserebuka..

Hapa ni Sufianimafoto, akiyarudi masebene na mchekeshaji wa Ze Commedy wa Chanel5, Masawe Mtata A.K.A Kicheko wakati wa Bonanza hilo.
Kwa Picha Zaidi  <<< BOFYA HAPA >>>
 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages