SIMBA NA YANGA ZABANWA NA FIFA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SIMBA NA YANGA ZABANWA NA FIFA

fifa logo FIFA to Test 10 Goal line Technology Systems
Na Ahadi Kakore
TIMU kongwe za soka nchini Simba na Yanga zimenyooshewa kidole na kutakiwa kufanya mabadiliko katika mfumo wa uendeshaji ili kuendana na dunia ya sasa kwenye mchezo huo.

Ofisa wa maendeleo wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Ashford Mamelodi, aliliambia Championi Jumatatu kuwa soka ya Tanzania inahitaji kufanyiwa mabadiliko makubwa.

“Simba na Yanga zinapaswa kuwa mfano, lazima yawepo mabadiliko kuanzia ngazi fulani. Ila hayawezi kuja kama mvua ila ni kufuata mfumo wa sasa ambao unaruhusu timu kama hizi zenye nguvu kuendeshwa kibiashara kuliko ilivyo hivi sasa,” alisema Mamelodi raia wa Botswana.

Akielezea juu ya tamko hilo Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, alisema: “Tumesikia kinachohitajika, tunachotakiwa kukifanya viongozi wa klabu ni kusimamia na kutekeleza kwa vitendo.”

“Tuna imani yatatusaidia kufanya mabadiliko yanayoeleweka na kutusogeza hapa tulipo na kwenda mbele zaidi,” alisema Louis Sendeu, msemaji wa Yanga.

Katika semina iliyoandaliwa na Fifa kwa maofisa wa klabu za ligi kuu nchini, klabu zimeshauriwa kujiendesha kibishara kwa mfumo wa kampuni ili kuendana na mfumo wa kisasa unaokuwa rahisi kuleta maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages