SAMATTA KUKIMBILIA ZAKE ULAYA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SAMATTA KUKIMBILIA ZAKE ULAYA

Na Khadija Mngwai
MSHAMBULIAJI kinda wa Simba, Mbwana Samatta (pichani), amesema yupo tayari kwenda kucheza Ulaya iwapo atapatikana wakala wa kumpeleka kucheza soka la kulipwa barani humo.

Samatta aliyetua Simba msimu huu akitokea African Lyon ameliambia Championi Jumatatu kuwa anajituma zaidi ili aweze kupata nafasi ya kusonga mbele kisoka kwa kuwa ndiyo mpango wake.

“Hakuna wakala yeyote aliyejitokeza kuhitaji kunipeleka nje, nina mpango wa kwenda nje iwapo atapatikana wa kufanya hivyo,” alisema Samatta na kuongeza:

“Nipo tayari kwenda nje, kwani mchezaji yeyote anajituma ili aweze kupata nafasi ya kucheza nje ya nchi kama ilivyo kwa wachezaji waliotangulia.”

Mshambuliaji huyo aliyejiunga Simba akitokea African Lyon amekuwa gumzo kutokana na kuonyesha kiwango cha juu katika siku za hivi karibuni ikiwa ni pamoja na kufunga mabao mechi za nyumbani na zile za kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages