MRISHO NGASA KUILIPA AZAM SH 98 MILIONI ZAO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MRISHO NGASA KUILIPA AZAM SH 98 MILIONI ZAO

 
Na Wilbert Molandi
IDADI ya mabao 11 aliyoifuingia timu yake ya Azam FC, Mrisho Ngassa (pichani), yamemfariji mchezaji huyo kutokana na thamani kubwa iliyotumika katika kumnunua ya shilingi milioni 98 kutoka Yanga mwanzoni mwa msimu huu.

Ngassa anasema anataka kuilipa Azam fedha hizo kwa kufunga mabao mengi, kwa kushirikiana vizuri na wenzake ili iwe bingwa au nafasi ya pili na kushiriki michuano ya kimataifa.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ngassa alisema suala la kuwa mfungaji bora  halimpasui kichwa. Anachotaka ni kuonyesha Azam FC haikukosea kumnunua kwa kiasi hicho kikubwa.

Kiungo huyo aliyewahi kuichezea Kagera alisisitiza kuwa, lengo la kufanikisha hilo ni kulinda thamani yake na kutimiza malengo ya Azam ya kumununua, ili kuiwezesha timu yake kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa na kitaifa.

“Nimenunuliwa Azam kwa ajili ya kuimarisha timu na siyo kingine, wapo wachezaji wengine  kwenye klabu hiyo, lakini wameniona ninafaa kwa ajili ya kuongeza nguvu. Nimepanga kulipa thamani yangu niliyonunuliwa nikitokea Yanga.

“Ninaamini nitafanikiwa malengo kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu pamoja na kocha wetu katika kukiandaa kikosi chake,” alisema Ngassa.

Ngassa aliyejiunga na Azam akitokea Yanga, anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji mzawa aliyenunuliwa kwa kiasi kikubwa kuliko wote nchini.

Kabla ya mechi za jana Azam ilikuwa ikishika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 32 nyuma ya Yanga yenye pointi 34 na Simba yenye 32.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages