NIZAR KHALIFAN KUIVAA TIMU YA TAIFA YA MAREKANI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NIZAR KHALIFAN KUIVAA TIMU YA TAIFA YA MAREKANI

 
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Vancouver Whitecaps FC anayoichezea Mtanzania, Nizar Khalfan juzi Jumamosi ilifanikiwa kutoka sare ya mabao 2-2, katika mechi ya kirafiki dhidi ya Timu ya Taifa ya Marekani chini ya umri wa miaka 18  kwenye Uwanja wa Avondale.

Katika mechi hiyo ambayo Nizar aliingia akichukua nafasi ya Bedri Gashi katika dakika ya 60, mabao ya Whitecaps yalipatikana kupitia kwa Long Tan lakini wapinzani hao walisawazisha kupitia kwa Robert Kristo na Aaron Kovar.

“Nadhani wachezaji walicheza katika kiwango kizuri, japokuwa sikufurahia tulivyocheza kipindi cha kwanza,” alisema Kocha wa Whitecaps, Teitur Thordarson.

Wachezaji wengi wa kikosi cha U-18 walikuwa ni wale walitoka katika kikosi cha U-17. Kikosi cha Whitecaps kilitarajiwa kuendelea na maandalizi kwa ajili ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS) inayotarajia kuanza hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages