Ndugu Zangu,
WaMisri wale hawakuchoshwa tu na Hosni Mubarak. Walichoshwa na mfumo mzima na hususan chama chao tawala. Ndio, tulishuhudia, kuwa jengo la kwanza kutiwa kiberiti na waandamanaji lilikuwa ni jengo la Makao Makuu ya Chama tawala cha nchi hiyo, NDP- National Democratic Party. Kilikuwa
chama kikongwe na kilichoshika hatamu za uongozi.
Kwa WaMisri, NDP kilikuwa ni chama walichokihofia hata katika maisha yao ya kila siku. National
Democratic Party kwa maana ya Chama Cha Taifa Cha Demokrasia hakikuwa cha Taifa na wala
Demokrasia ndani yake. Kilikuwa chama cha wateule wachache akiwemo mwana wa Hosni Mubarak
aitwaye Gamal Mubarak aliyepewa cheo cha Ukatibu Mkuu na aliandaliwa na baba yake kumrithi
madaraka ya Urais.
Ni lipi jema kwa mtawala na chama; kuhofiwa au kupendwa? Mwingine angependa vyote, lakini
haiwezekani. Na hilo ni Neno La Leo.
Maggid,
Iringa,
Februari 16, 2011
http://mjengwa.blogspot.com

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)