KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe (pichani) jana alitangaza Baraza la Mawaziri Kivuli likiwa na mawaziri 29 wote kutoka Chadema, huku akimtosa Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda (pichani chini).
Shibuda ambaye aliyehamia Chadema baada ya kutoswa kwenye kura za maoni ndani ya CCM, ameonekana kuwa na toifauti za kimtizamo dhidi ya chama chake cha sasa hali inayoweza kuwa ndiyo imechangia kutokuwamo kwenye Baraza la Mawaziri Kivuli.
Katika Baraza hilo, Mbowe amewateua Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuwa Waziri Kivuli wa Fedha, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika kuwa Waziri Kivuli wa Nishati na Madini na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuwa Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Wizara ya Fedha na Uchumi inayoongozwa na Waziri Mustapha Mkullo, ndiyo muhimili wa uchumi wa nchi, ikishughulikia masuala yote yanayohusu mipango na bajeti, wakati Wizara ya Nishati na Madini inayoongozwa na Waziri William Ngeleja inabeba uzito mkubwa kwa sasa kutokana na kuwapo kasoro kadhaa za kiuendeshaji ambazo zimekuwa zikigusa sekta zote muhimu za uchumi wa nchi na maendeleo.
Changamoto kubwa katika wizara hiyo ni matatizo makubwa ya uhaba wa nishati ya umeme, ambayo kwa sasa yamesababisha kuwapo kwa mgawo wa umeme wa muda mrefu, huku sekta ya madini ikilaumiwa kwa kutowanufaisha Watanzania na badala yake kuwanufaisha wageni kutokana na udhaifu wa sheria pia mikataba baina ya Serikali na wawekezaji.

Kwa Habari Zaidi <<<<<BOFYA HAPA>>>>>
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)