KAMATI YA BUNGE YA USALAMA CHINI YA MWENYEKITI WAKE EDWARD LOWASA WATEMBELEA GONGO LA MBOTO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KAMATI YA BUNGE YA USALAMA CHINI YA MWENYEKITI WAKE EDWARD LOWASA WATEMBELEA GONGO LA MBOTO

SPIKA wa Bunge Anna Makinda akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, hundi ya Sh. milioni 37.80,  leo, kweye kituo cha uratibu na kupokea misaada kwa ajili ya waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto, kilichopo, Ofisi ya Mtendaji Kata ya Ukonga.Fedha hizo zimetolewa na wabunge kwa kusaidia wananchi walioathirika ma mabomu hayo. Kulia ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Mecky Sadiki.
 MWENYEKITI wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa mkoa huo, Saidi Mecky Sadiki (kushoto), akitoa taarifa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, kuhusu  mwenendo na hatua zilizochukuliwa na serikali ya mkoa huo, dhidi ya maafa ya milipuko ya mabomu ya Gongo la Mboto,Waziri Nahodha alipotembelea kituo cha  tathmini na kupokea misaada kwa waathirika wa mabomu hayo, kilichopo Ofisi ya Mtendaji Kata ya Ukonga, leo. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inpekta Jenerali, Saidi Mwema
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Edward Lowassa, akikaribishwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, yeye na kamati hiyo walipotembelea leo, kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzaniani, Gongo la Mboto, Dar es Salaam, kufahamu mazingira na hasara ya milipuko ya mabomu iliyotokea katika ghala la silaha la JWTZ katika kambi hiyo, Jumatano iliyopita.Picha na Bashir Nkromo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages