DEWJI: LAZIMA TP MAZEMBE WAFUNGIKE TU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

DEWJI: LAZIMA TP MAZEMBE WAFUNGIKE TU

Na Khadija Mngwai
MDAU wa soka, Kassim Dewji (pichani), amesema Simba wana uwezo wa kuwafunga mabingwa wa Afrika, TP Mazembe, kutoka DR Congo na kusonga mbele lakini akaonya haitakuwa kazi rahisi.

Dewji, Katibu Mkuu wa zamani wa Simba aliwahi kuwaongoza Wekundu wa Msimbazi, kuwang’oa mabingwa na timu bora wa Afrika, Zamalek, nyumbani kwao Cairo, Misri.

Simba inakumbana na vigogo TP Mazembe katika mechi ijayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwang’oa Elan Club ya Comoro kwa kuwachapa jumla ya mabao 4-2.

Akizungumza na Championi, Dewji alisema: “Ni lazima tuishinde Mazembe ingawa utakuwa ni mchezo mgumu sana.

Ninaamini viongozi wa Simba ni makini na wataichukulia mechi hiyo kwa umakini zaidi tofauti na ligi kuu.

“Kunahitajika juhudi za ziada kuanzia sasa ili kuiweka sawa timu, kwa viongozi kuchukulia uzito wa timu tutakayokutana nayo ambao ni mabingwa watetezi,” alisema Dewji.

Alifafanua kuwa matokeo ya mchezo dhidi ya Toto African ya sare ya mabao 2-2 yalitokana na  Simba kutoitilia uzito mechi hiyo lakini anaamini hawatofanya hivyo katika mechi ya Mazembe itakayopigwa Machi 19.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages