RAISI JAKAYA KIKWETE AZINDUA UCHANGIAJI KITUO CHA WANAFUNZI UDSM USIKU WA KUAMKIA LEO IKULU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RAISI JAKAYA KIKWETE AZINDUA UCHANGIAJI KITUO CHA WANAFUNZI UDSM USIKU WA KUAMKIA LEO IKULU



Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Waziri mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba wakati wa hafla ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Wanafunzi uliofanyika ikulu jijini Dare s salaam jana usiku.Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala.Zaidi ya shilingi Bilioni 1.6 zilikusanywa katika hafla hiyo ya uzinduzi ambapo Rais Dr.Jakaya kikwete alichangia jumla ya Shilingi milioni kumi.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mchango wa Shilingi elfu kumi kutoka kwa mpigapicha wa gazeti la Jamboleo Richard Mwaikenda wakati wa hafla ya uzinduzi wa kuchangia ujenzi wa kituo cha wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana.Zaidi ya shilingi Bilioni 1.6 zilikusanywa katika hafla hiyo ya uzinduzi ambapo Rais Dr.Jakaya Kikwete alichangia jumla ya shilingi milioni kumi.Picha na Freddy Maro-IKULU

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages