MH AZZAN: NAMZIMIKIA SANA JENNIPHER - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MH AZZAN: NAMZIMIKIA SANA JENNIPHER

 
Na Brighton Masalu
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Mhe. Iddi Azzan amemmwagia sifa na kusema mtoto anayezidi kuwashangaza Watanzania wengi katika tasnia ya filamu za Bongo, Hannifa Daud ‘Jennifer’ (pichani) na kueleza kuwa siku zijazo atatisha.

Jennifer alipewa sifa na mheshimiwa huyo, Jumanne iliyopita wakati kiongozi huyo alipokuwa akihojiwa katika Kipindi cha Take One, kinachorushwa hewani na Runinga ya Clouds  chini ya Mtangazaji Zamarad Mketema.

Mbunge huyo alisema kuwa, filamu ambayo imemfanya azidi kumpenda msanii huyo ‘kinda’, ni ile iitwayo ‘Uncle JJ’ ambapo mtoto huyo alionesha kiwango cha juu mno cha uigizaji.

“Siyo siri, mtoto huyu ananifurahisha sana katika uigizaji wake, maana anapoigiza ‘sini’ ya kiburi, ki ukweli huvaa uhalisia unaotakiwa, siku zijazo lazima atatisha,” alisema  Azzan na kuongeza;

“ Ni kweli kwamba wasanii wetu wanajitahidi sana katika filamu zao, hasa ukiangalia mazingira ya kazi zao katika kuigiza ambayo bado ni magumu,

lakini nawaomba wasikate tamaa badala yake wazidi kuongeza bidii na wawe makini na kazi yao, hakika watafanikiwa.”

Mbunge  Azzan amekuwa ni kiongozi wa serikali anayefuatilia zaidi masuala ya sanaa hapa nchini, jambo linalopaswa kuigwa na viongozi wengine, ili kuwapa moyo wasanii wetu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages