NDEGE YA RAISI YENYE UTATA YAPELEKWA MAREKANI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NDEGE YA RAISI YENYE UTATA YAPELEKWA MAREKANI

 
Na Haruni Sanchawa
NDEGE aina ya Gulfstream 550 (pichani) iliyonunuliwa  na  serikali kwa Shilingi bilioni 40 kwa ajili ya  matumizi  ya  Rais  na kuleta utata na mjadala mkubwa miongoni mwa wananchi, imepelekwa Marekani, Uwazi limegundua.

Uchunguzi  uliofanywa  na  gazeti  hili  katika  idara  zinazohusika na usimamizi wa ndege hiyo,   umebaini kuwa  kwa  sasa haipo nchini na iko   Marekani kwa ajili ya matengenezo tangu mwaka jana.

Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, inadaiwa ndege  hiyo ilinunuliwa ikiwa mbovu.

Mwandishi wetu alikwenda Ofisi za Mamlaka ya Wakala wa Ndege za Serikali ili kupata ufafanuzi zaidi lakini alijibiwa kuwa mkurugenzi mkuu hakuwepo ofisini.

Hata hivyo, afisa mmoja ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini kwa kuwa si msemaji, alikiri ndege hiyo kuwa nje ya nchi kwa ajili ya matengezo  na kuongeza kuwa ni  utaratibu ambao upo hata kama haijafanya kazi yoyote.

Mara baada ya ndege hiyo kununuliwa enzi za utawala wa Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kuliibuka malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali ambao walisema ilinunuliwa kwa fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kwa maendeleo ya taifa hususan ujenzi wa shule, hospitali nk lakini hoja hizo zilipuuzwa.
Kwa Hisani Ya GLOBAL PUBLISHER TANZANIA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages