KAMPUNI YA TTCL YAOMBA UDHAMINI WA SERIKALI KUPATA MIKOPO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KAMPUNI YA TTCL YAOMBA UDHAMINI WA SERIKALI KUPATA MIKOPO


 Katibu Mkuu wa (TEWUTA) Bw Junas Ndaro akiongea na waandishi wa Habari
------
 
Chama cha wafanyakazi kwenye sekta ya mawasiliano nchini(TEWUTA)kimeiomba serikali kukubali kusaini mkataba wa kuipa udhamini kampuni ya simu tanzania (TTCL)ili kuweza kupata mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha nchini

 Katibu Mkuu wa (TEWUTA) Bw Junas Ndaro akiongea na waandishi wa Habari na kueleza kusikitishwa kwake na taarifa moja iliyotolewa na moja ya magazeti hapa nchini la taerehe 24/12/2010 lilokua na kichwa acha habari kilichosomeka ''Makampuni kama TTCL yasipewa nafasi ya kuwakamua walipa kodi"

Akifafanua kuhukauli hiyo Bw Ndaro amesema, gazeti hilo liliandika habari yeney mtazamo hasi bila kuelewa kuwa TTCL haihitaji fedha za wananchi badala yake inahitaji dhamana ya serikali ili iweze kukopa  na kujiimarisha kibiashara.

'' TTCL toka kipibndi cha ubinafsishaji wake imepata misukosuko mingi na kusababisha kupoteza mwelekeo wa kibiashara na hivyto tunaomba dhamana ya serikali na si fedha za serikali ili kuweza kuhimili vishindo vya ushindani wa kibiashara kwenye sekta ya mawasiliano nchini'. alisema Ndaro.

Chama cha wafanyakazi kwenye sekta ya mawasiliano nchini(TEWUTA)kimeiomba serikali kukubali kusaini mkataba wa kuipa udhamini kampuni ya simu tanzania (TTCL)ili kuweza kupata mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha nchini.

Habari hii na Mary Kweka-MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages