WAZIRI MKUU Mizengo Pinda
----
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameonyesha kwa vitendo kuwa yeye ni mtoto wa mkulima baada ya kukataa gari jipya ka kifahari alilonunuliwa na wasaidizi wake kwa akisema kwamba alilonalo linamtosha.
----
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameonyesha kwa vitendo kuwa yeye ni mtoto wa mkulima baada ya kukataa gari jipya ka kifahari alilonunuliwa na wasaidizi wake kwa akisema kwamba alilonalo linamtosha.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana jioni kwa njia ya simu, Pinda alisema kuwa uamuzi huo aliuchukua mwaka huu kabla ya uchaguzi mkuu kuanza baada ya kukataa kulitumia gari jipya aina ya Landcruiser VX 8 lenye thamani ya sh milioni 280.
Alisema kuwa aliamua kukata kulitumia gari hilo baada ya kungundua kuwa alilonalo ambalo ni la bei ndogo kuliko hiyo bado lina uwezo.
"Ni kweli nimelikataa kulitumia gari hilo kwani niliona hata gari hili ambalo nimeanza nalo kulitumia kama mawaziri mkuu bado halikuwa na matatizo, sasa kwa nini nipewe jingine jipya, hii itakuwa ni matumizi mabaya fedha za serikali," alisema.
Alisema baada ya kulikataa kulitumia gari hilo aliwaagiza watalaam wake kwa sababu tayari walishalinunua kumtafuta mtu mwingine wa kumpa kulitumia, lakini kama angeshirikishwa katika mchakato wa awali angewakubalia
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)