Pichani ndio washindi ama vinara wa Tusker Project Fame 2010,Kulia ni David kutoka nchini Uganda ambaye ameibuka nafasi ya kwanza na Peter Msechu kutoka nchini Tanzania ameibuka nafasi ya pili.
Sisi Tanzania Msechu ndio mshindi wetu wa Tusker Project Fame 2010, kwa sababu ametutoa kimasomaso kwa kiasi kikubwa hasa ukichukulia washiriki wenzake kutoka hapa Tanzania walitolewa mapema,lakini yeye Peter Msechu kapigana kiume na hatimaye kufanya vyema na kuibuka na nafasi ya pili ambayo kimsingi si ya kubeza hata kidogo,bado ni ushindi tosha kabisa kwetu.
Karibu nyumbani Peter Msechu ukiwa kifua mbele kabisa huku watanzania wenzako tukiamini kuwa ndio mshindi wetu wa Tusker Project Fame 2010.
Shindano la Tusker Project Fame safari hii linafanyika ikiwa ni awamu ya nne,likiwa limeshilikisha nchi kadhaa ikiwemo Kenya,Uganda,Rwanda,Tanzania pamoja na Sudan ya kusini.
Habari Kwa Hisani Ya Michuzi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)