Zaina Malongo
KILIO cha wananchi kupinga kupanda kwa bei ya umeme, sasa kimehamia kwenye moja ya makundi makubwa na yenye nguvu baada ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(Tucta) kuandaa maandamano nchi nzima kupinga bei mpya. Tayari Chadema imeshatangaza kuandaa maandamano nchi nzima kupinga bei hiyo mpya ya umeme ambayo ni ongezeko la asilimia 18 na ambalo limeshapingwa na wananchi wa kada mbalimbali.
Mbali na ongezeko hilo, Tanesco pia imetangaza mgawo wa umeme utakaokuwa wa kuanzia masaa matano hadi 10 kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia jana, uamuzi ambao umetafsiriwa kuwa utaongeza makali ya maisha. Katibu mkuu wa Tucta, Nicholas Mgaya alisema watafanya maandamano ya amani kupinga kupanda kwa umeme kutokana na athari zake ambazo alisema ni pamoja na kusababisha ugumu wa maisha na umasiki kwa wafanyakazi.

“Serikali isipandishe bei ya umeme bali itafute njia nyingine za kuzuia tatizo hilo kutokana na athari kubwa zitakazowalenga wafanyakazi pamoja na kuliweka taifa katika janga la umasikini,” alisema Mgaya. Mgaya alisema nchi kama ya Tanzania, ambayo ina vyanzo vya maji kama vile maziwa na mito, ikitumia rasilimali hizo kwa umakini, inaweza kuondoa tatizo la umeme. “Kama serikali haitachukua tahadhari katika kipindi hiki, hapo baadaye kutakuwa na mwelekeo mbaya hasa kwa wananchi kukosa umeme kabisa,” alisema Mgaya.
Alisema kamati ya utendaji wa Tucta iliyokutana juzi katika kikao cha kawaida, iliazimia kuwa itoe taarifa kwa serikali ya kupinga kupanda kwa bei ya umeme. Alisema hatua hiyo ni kutokana na kwamba hata bei ya sasa iko juu na hivyo kuwafanya wananchi washindwe kuimudu. “ Hivi sasa kuna watu hawatumii baadhi ya vifaa vya umeme kutokana na ukubwa wa bei, je ikipanda tena si watashindwa hata kuwasha taa,” alisema. Takwimu zinaonyesha kuwa ni asilimia 12 ya Watanzania ndio wanaotumia umeme majumbani, lakini kutokana na umuhimu wa nishati hiyo katika uzalishaji, kupanda kwa bei ya umeme kunaweza kusababisha gharama za maisha kupanda.
Tanesco inategemea kuzalisha umeme kutokana na mitambo inayoendeshwa kwa maji, gesi na dizeli.
Akitangaza uamuzi wa kupandisha bei ya umeme, mkurugenzi wa Ewura, Haruna Masebu aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa ongezeko hilo la bei ni chini ya mapendekezo ya Tanesco kwa asilimia 16.1.

Kwa taarifa Zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)