WAZIRI wa Uchukuzi, Omari Nundu ameitaka Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), kusitisha mkataba wake na Kampuni ya udalali ya Majembe ifikapo Desemba 31 mwaka huu.
Taarifa hiyo itakuwa ya furaha kwa madereva wa mabasi yafanyayo safari zake ndani ya miji na yale yaendayo mikoani baada ya kupambana na maofisa wa Majembe kwa muda mrefu, wakilipishwa faini kubwa, kuwekwa mahabusu na kuzuiwa kufanya shughuli zao kwa muda mrefu na hivyo kupunguza "hesabu".
Wamiliki na madereva wa mabasi walipinga mara kadhaa uamuzi wa Sumatra kuitumia kampuni hiyo na wakati mwingine kuendesha migomo ya kutoa huduma za usafiri, wakidai kuwa maofisa wa kampuni hiyo ya udalali hawaelewi vizuri masharti ya leseni za usafirishaji. Walidai kuwa maofisa hao wa Majembe waliwalipisha hadi faini ya Sh250,000 kwa madai ya kufanya makosa ya kukiuka masharti ya leseni, na kushauri polisi ndio waendelee na jukumu lao la kawaida la kusimamia sheria hizo.

Kwa Taarifa Zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)