KILIMANJARO STARS YATINGA FAINALI BAADA YA KUIGALAGAZA THE CRANE 5-4 KWA MIKWAJU YA PENATI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KILIMANJARO STARS YATINGA FAINALI BAADA YA KUIGALAGAZA THE CRANE 5-4 KWA MIKWAJU YA PENATI

Wachezaji wa timu ya Kilimanjaro Stars wakishangilia ushindi walioupata dhidi ya Ugannda 'The Craners' kwa mikwaju ya penati 5-4 na kupata tiketi ya kuingia fainali ya mashindano ya Tusker Challange Cup katika mchezo uliopigwa jioni ya jana ndani ya Uwanja wa Taifa,jijini Dar.
Kocha wa Makipa wa Kilimanjaro Stars,Juma Pondamali akiyarudi magoma na Ramadhan Shamte mara baada ya ushindi mnono wa timu hiyo dhidi ya Uganda.kwa matokeo hayo Kilimanjaro Stars itamenyana na Ivory Coast katika fainali ya mashindano ya Tusker Challange Cup hapo jumapili ya Desemba 12.
furaha ilitawala kwa mashabiki wa Kilimanjaro Stars.
Waliofunga upande wa Uganda ni Issack Isinde, Dan Walusimbi, Emmanuel Okwi na Andy Mwesigwa
Kilimanjaro Stars waliofunga ni Nsajigwa Shadrack, Stephano Mwasika, Shaaban Nditi, Salum Machaku na Erasto Nyoni.
Nahodha wa Kilimanjaro Stars,Shadrack Nsajigwa (Fusso) akimfariji Golikipa wa Uganda mara baada ya kufungwa penati zote na kuipa ushindi Kilimanjaro Stars.
Kipa wa Kilimanjaro Stars,Juma Kaseja akipangua moja ya penati zilizopigwa na wapinzani wao Uganda.
Kipa wa Uganda,Odongkala Robert akishika kichwa na kujilaumu mara baada ya kufungwa penati ya mwisho na kuipatia nafasi timu ya Kilimanjaro kuitinga fainali kwa madaha yote.
Benchi la Kilimanjaro Stars.
Benchi la Uganda ‘ The Craners’.
Nahodha wa timu na Kilimanjaro,Shadrack Nsajigwa akijaribu kumtoka beki wa Uganda,Walusimbi Godfrey katika mtanange uliopigwa leo ndani ya Uwanja wa Taifa,jijini Dar.Kilimanjaro Stars imeshindwa kwa penati bao 5-4.
Mrisho Ngassa wa Kilimanjaro Stars akitafuta namna ya kumtoka beki wa Uganda,Walusimbi Godfrey katika mtanange uliopigwa jioni ya jana ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages