TWIGA STAR YALALA 2-3 DHIDI YA MALI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TWIGA STAR YALALA 2-3 DHIDI YA MALI

TWIGA STAR YALALA 2-3 DHIDI YA TIMU YA MALI
Kocha wa Twiga Stars Charles Boniface
Mkwassa na wachezaji wake

Timu ya taifa ya Tanzania Wanawake Twiga Stars imefungwa magoli 3-2 na timu ya taifa ya Mali katika mchezo wao uliofanyika nchini Afrika Kusini jioni ya Jana.

Mchezo huo ulikuwa ni wa pili katika mashindano ya kombe la mataifa huru ya Afrika kwa wanawake, ambapo mchezo wa kwanza Twiga Stars ilifungwa magoli 2-1 na timu ya wanawake ya Afrika Kusini BanyanaBanyana.

Hivi sasa timu hiyo inakabiliwa na mtihani mwingine wakati itakapocheza na timu ya taifa ya Nigeria na kutokana na vipigo hivyo viwili timu hiyo itacheza mchezo huu kama kukamilisha ratiba tu kwani kwa kufungwa mara mbili tayari imeshapoteza matumaini ya kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages