SAMWEL SITA NA HAMU YA KUONGOZA BUNGE JIPYA LENYE USHINDANI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SAMWEL SITA NA HAMU YA KUONGOZA BUNGE JIPYA LENYE USHINDANI

Samwel Sitta:Na Hamu ya Kuongoza Bunge Lijalo lenye Upinzani Wenye Uwezo Mkubwa Kisiasa
ALIYEKUWA Spika wa Bunge la Tanzania Samuel Sitta
-------
Na Msibe Beda Lukwangule
ALIYEKUWA Spika wa Bunge la Tanzania lililomaliza muda wake,Samuel Sitta,ana hamu ya kuliongoza Bunge lijalo hivyo anatarajia kujaza fomu kesho kukiomba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimpitishe agombee uspika.

Sitta amesema, anafahamu kuwa Bunge lijalo litakuwa na changamoto zaidi kuliko lililopita,lakini ana uwezo na uzoefu wa uongozi hivyo atalimudu Bunge hilo la 10 la Tanzania.Mwanasiasa huyo amesema,atafurahi kama atakuwa Spika wa Bunge lenye changamoto nyingi kama Bunge lijalo.“Kwa kweli nadhani niseme wazi tu,wakati wangu ndiyo umefika”amesema Sitta wakati anahojiwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV na Redio One Stereo saa kadhaa baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa ubunge jimbo la Urambo Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)

Alisema,anafahamu kwamba kutakuwa na wabunge wa kambi ya upinzani wenye uwezo mkubwa kisiasa, yupo tayari kuwaongoza, na pia atakaa vizuri na wabunge machachari ili kusiwe na vurugu bungeni.“Hatuwezi kuwa na ukiritimba wa chama kimoja au viwili halafu tukasema hiyo ndiyo demokrasia…mimi natarajia tutaenda vizuri hasa wakinichagua kuwa Spika”alisema Sitta .

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages