MUSTAFA JAFFER SABODO:Kada wa CCM anayesaidia vyama vya siasa kukuza Demokrasia
Imeandikwa na Kaanaeli KaalePichani ni Mustafa Jaffer Sabodo,mfanyabiashara maarufu na muumini wa falsafa za Baba wa Taifa,hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,mwasisi wa Taifa hili.
HAIKUWA mara yake ya kwanza kupamba kurasa za vyombo vya habari,kwani amekuwa akifanya hivyo miaka nenda miaka rudi kutokana na umaarufu wake mkubwa.
Lakini kitendo cha kukimwagia mamilioni ya shilingi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), tena katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu unaofanyika leo kote nchini, kiliwaacha wengi midogo wazi; hasa kutokana na ukweli kwamba, aliyefanya hivyo ni mkereketwa wa kweli wa chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hapa tunamzungumzia Mustafa Jaffer Sabodo,mfanyabiashara maarufu na muumini wa falsafa za Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,mwasisi wa Taifa hili.
Mwenyewe, bila ya kutafuna maneno amelisisitizia gazeti hili kuwa, hakukosea kuipatia Chadema Sh milioni 200 za kampeni, akidai anadhani ni wakati mwafaka wa kuvisaidia vyama vya upinzani viweze kupata uwakilishi utakaokuwa unaiamsha serikali pale itakapotokea imesinzia.
Katika mazungumzo na mwandishi wa makala haya katikati ya wiki hii; Sabodo alisema: “Katika uchaguzi mkuu wa Jumapili ijayo (leo),ni wazi kwamba hivi sasa vyama vya upinzani haviwezi kuingia madarakani kwa sababu bado ni vichanga mno.kwa mengi zaidi bofya na Endelea.............>>>>>
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)