Dr. Shein Ala Kiapo Leo Zanzibar. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Dr. Shein Ala Kiapo Leo Zanzibar.

Dr. Shein Aapishwa Zanzibar Leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr. Ali Mohamed Shein akila kiapo cha kuiongoza Serikali ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein akila kiapo cha urais mbele ya jaji mkuu wa Zanzibar Hamid Mahamoud(kushoto) wakati wa sherehe za kumuapisha zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Amaan Stadium mjini Zanzibar leo asubuhi.Katikati anayeshuhudia ni rais wa Zanzibar aliyemaliza muda wake Amani Abeid Karume.
Rais Wa Zanzibar aliyemaliza muda wake Amani Abeid Karume akimpongeza na kumkabidhi miongozo ya kazi Rais Mpya wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein wakati wa sherehe za kuapishwa zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Amaan mjini Zanzibar leo asubuhi.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akilihutubia Taifa katika sherehe za kuapishwa kwake kuwa Rais wa awamu ya saba wa Zanzibar katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Amani Zanzibar leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikaguwa gwaride la vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama, baada ya kula kiapo kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Amani leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais mpya wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya Dr.Shein kuapishwa mjini Zanzibar leo asubuhi.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akimpongeza mumewe Dr.Ali Mohamed Shein muda mfuoi baada ya Dr.Shein kuapishwa kuwa Rais Mpya wa Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mshindi wa pili katikA KINYANG’ANYIRO cha urais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad wakati wa sherehe za kumuapisha Rais mpya wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimaina na mgombea Mwenza Dr.Mohamed Gharib Bilal katika uwanja wa michezo wa Amaan mjini Zanzibar wakati wa sherehe za kumuapisha Rais mpya wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein leo asubuhi.Katikati ni Mshindi wa pili katika mbio za urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Maalim Seif Shariff Hamad.
Sehemu maalum iliyoandaliwa rasmi kwa kuapishwa kwa Rais Mpya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dr. Ali Mohamed Shein.
Vikosi mbali mbali vilivyoshiriki katika gwaride la kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar,kikiondoka uwanjani hapo.
Wananchi na wanachama wa vyama mbalimbali wakiwa katika sherehe ya kuapishwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein zilizofanyika leo katika uwanja wa Amani.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages