- LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mambo yalivyokua Kwenye Ofisi Kuu ya Halmashauri ya Mwanza Jana
HALI JINSI ILIVYOKUWA KWA SIKU YA JANA HATUA KWA HATUA MASAA YAKIYOYOMA.
WANANCHI HAO WALIANZA KURUSHA MAWE KTK OFISI HIZO ZA JIJI NA HATIMAYE WAKAVUNJA UPANDE MMOJA WA KUSHIKILIA GETI KUU LA KUINGIA OFISI HIZO HALI ILIYOSABABISHA GETI KUKOSA BALANCE HIVYO WAO KUPENYA KIRAHISI NA KUKARIBIA ENEO LA TUKIO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA SIMON SIRO ALIWASIHI WANANCHI KUWA WATULIVU NA KUTOFANYA VURUGU KWANI JESHI HILO LIKO MAHALI HAPO KULINDA AMANI NA USALAMA HUKU LIKI HAKIKISHA ZOEZI HILO KUWA LINAFANYIKA KWA HAKI NA WANANCHI KUSHEREHEKEA USHINDI WAO KWA AMANI.
MOJA YA MAGARI OFISINI HAPO YALIYODHURIKA
MOJA YA ATHARI ZILIZOJITOKEZA NI KUCHOMWA MOTO KWA OFISI ZA CCM KITUO CHA NELA NA KUTEKETEA KABISA ZIMAMOTO IKISHINDWA KUFIKA ENEO HILO KUTOKANA NA VURUGU NA MAWE MAKUBWA YALIYOTANDAZWA BARABARANI.
MGOMBEA UBUNGE WILAYA YA NAYMAGANA BW. WENJWE AKIWATULIZA WANACHAMA WAKE KUWA WATULIVU NA KUYASUBIRI MATOKEO RASMI MARA BAADA YA UHAKIKI KUFANYIKA INGAWA TAYARI KULIKUWA NA DALILI ZA WATU KUCHOKA KUYASUBIRI MATOKEO HAPA ILIKUWA SAA NANE NA DK 45 MCHANA.
HALI YA VURUGU ILITULIA MAJIRA YA SAA 1USIKU MARA BAADA YA MATOKEO KUTANGAZWA NAE MSIMAMIZI WA UCHAGUZI MWANZA AMBAYE PIA NI MKURUGENZI WA JIJI BW. WILSON KABWE. NYAMAGANA UBUNGE UMEKWENDA KWA BW. WENJE WA CHADEMA ALIYEPATA KURA 38,871 AKIMWANGUSHA BW.LAURANCE MASHA ALIYEPATA KURA 27,883 KURA ZILIZOPIGWA ZILIKUWA 67,560 WALIOJIANDIKISHA 189,976. KWA UPANDE WA ILEMELA MGOMBEA WA CHADEMA BW. HAINES SAMSON (KURA 31,296)AMEMBWAGA ANTHONY DIALO WA CCM (KURA 26,870).PICHA ZOTE KWA MSAADA WA MDAU ALBERT SENGO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages