NEC KUTANGAZA MAJINA LEO YA WABUNGE VITI MAALUMU. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NEC KUTANGAZA MAJINA LEO YA WABUNGE VITI MAALUMU.

NEC kutangaza leo Majina ya Wabunge Viti Maalum
Mweny-ekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Lewis Makame
----------
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema leo inataweka wazi majina ya wabunge wa viti maalum baada ya kukamilisha taratibu zote, ikiwemo vyama vya siasa kuwasilisha kwao majina ya walioomba nafasi hizo.

Akizungumza na gazeti la NIPASHE jana,Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Lewis Makame, alisema leo watakutana kwa ajili ya kukamilisha uteuzi huo na kukabidhi majina katika ofisi ya Bunge kwa ajili ya kuapishwa na wenzao waliochaguliwa kwenye majimbo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31, 2010.

Alisema kilichokuwa kikifanyika baada ya kumalizika Uchaguzi Mkuu ni kupiga mahesabu ya kila chama kipate nafasi ngapi kulingana na wingi wa kura ambazo kila chama kilipata. Aliongeza kuwa kuna nafasi 102 za wabunge wa viti maalum vya wanawake na kwamba kila chama kitapata kulingana na idadi ya kura walizopata kwa upande wa wagombea wa urais pamoja na idadi ya wabunge wa majimbo waliopata.
Mwaka huu Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepata wabunge wa majimbo 186 ambapo mwaka 2005 walikuwa 205 Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) imejizolea wabunge 22, mwaka 2005 ilipata 5, Chama Cha Wananchi (CUF) kilipata wabunge(24) UDP mbunge mmoja na NCCR Mageuzi wanne.Chama kingine kilichopata wabunge ni Tanzania Labour Party (TLP) ambacho kilipata jimbo moja la Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Mwaka 2005 CCM ilipata wabunge 59 wa viti maalumu,CHADEMA viti 6,CUF ikapata nafasi hizo 13.Mwaka huu idadi ya wabunge kutoka kambi ya upinzani itaongezeka katika Bunge lijalo.Habari hii na Vincent Makore
Kwa Hisani Ya Haki Ngowi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages