SERIKALI YA SWEDEN YAIPA TAFU TANZANIA SH BILIONI 4 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SERIKALI YA SWEDEN YAIPA TAFU TANZANIA SH BILIONI 4

SERIKALI ya Sweden imetoa msaada wa Sh. Bilioni 44 kwa Tanzania ili kuboresha Huduma za Usambazaji Umeme Vijijini
PICHANI Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhani Kijjah (kushoto) akizungumza kabla ya kutia saini.Kulia ni Kiongozi wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Sweden, Erik Korsgren.Picha na Vicent Tiganya
--------------
SERIKALI ya Sweden imetoa msaada wa Sh. Bilioni 44 kwa Tanzania kwa ajili ya kuimarisha na kuboresha huduma za usambazaji umeme vijijini zinazotekelezwa na mfuko wa usambazaji wa umeme vijijini (REA).Hadi sasa REA imepeleka umeme katika wilaya 11 na wanaendeleza shughuli hizo katika mikoa 16 nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhani Kijjah kwa pamoja na Kiongozi wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Sweden, Erik Korsgren walisaini makubaliano ya kusaidia mradi huo wa umeme vijijini, katika hafla iliyofanyika jana Dar es Salaam. Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo, Kijjah alisema serikali hiyo imekubali kuisaidia Tanzania ili kuwezesha REA kupanua na kutekeleza shughuli za umeme vijijini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages